Wednesday 2 November 2016

team ndo zimesababisha wa TZ kukosa tuzo

Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy model huyo wa wimbo wa ‘Salome’ amesema kuwa team ndizo zilizochangia Tanzania ishindwe kupata hata tuzo moja.
“Unajua kwanza sisi Tanzania tuna team, kwahiyo team zinakuwa kama zinatutenganisha, kama zile team zote zingekuwa kitu kimoja labda watanzania wote tungeweza kushinda. Kuna watanzania wengine wanadiriki kuwapigia promo Instagram wanigeria washinde wao,” amesema Mobetto.
Mwanamitindo huyo ameongeza kuwa team hizi zingekuwa na faida kama zingekuwa zinaungana kwenye kitu cha kuiwakilisha nchi. Tazama mahojiano hayo hapa chini.

No comments:

Post a Comment