Afrimma 2016
Staa wa Bongo Fleva nchini, Harmonize (kushoto) akiwa na staa wa muziki wa Nigeria, Tekno.
Wengine waliochukua tuzo ni Wakenya, Sauti Sol walioshinda kundi bora
la muziki Afrika ikiwa ni tuzo iliyokua ikiwaniwa na Radio na Weasel wa
Uganda, Os Moikanos wa Angola, Bracket wa Nigeria, Mi Casa South
Africa, R2bees wa Ghana, Bana C4 wa Congo DRC na Yamoto Band wa
Tanzania.Mkenya Akothee ameshinda msanii bora wa kike Afrika Mashariki, tuzo iliyokua inawaniwa na Victoria Kimani wa Kenya, Vanessa Mdee na Linah wa Tanzania, Aster Aweke na Tsedenia wa Ethiopia, Knowles wa Rwanda na Sheebah Karungi wa Uganda.
Mkenya mwingine ni staa wa Gospel Kenya Willy Paul ambaye ameshinda tuzo ya Best Gospel Act iliyokua ikiwaniwa na Frank, Uche, Sinach wa Nigeria, SP Koffi na Sonnie wa Ghana, Icha wa Congo na Ntokozo wa South Africa.
No comments:
Post a Comment